WAFANYIBIASHARA WALALAMIKIA UCHAFU KATIKA SOKO LA KONGELAI.

Na Benson Aswani
Wafanyibiashara katika soko la Kongelai katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamelalamikia uchafu katika soko hilo hali wanayodai huenda imesababishwa na mishahara duni wanayolipwa wanaoendeleza usafi katika soko hilo.
Wakiongozwa na Nelly Pushe wafanyibiashara hao aidha wamelalamikia ukosefu wa jaa la kutupa taka katika soko hilo huku wakitoa wito kwa gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo kuangazia hali ya soko hilo ili kuwahakikishia mazingira bora ya kuendeleza shughuli zao.
Wafanyibiashara hao wamesema kuwa wamelazimika kufanyia shughuli zao katika mazingira machafu licha ya kulipia ushuru.