WAFANYIBIASHARA WAELEZEA HOFU YA KUENEA VIRUSI VYA CORONA KONGELAI.
Wafanyibiashara katika soko la Kongelai kaunti hii ya Pokot magharibi wameelezea wasiwasi wa kuenea virusi vya corona eneo hilo kutokana na kutangamana wakazi wengi bila kuzingatia kanuni za kukabili maambukizi ya virusi hivyo.
Wakiongozwa na Rosana Kashol wafanyibiashara hao wamesema kuwa raia kutoka taifa jirani la Uganda na kaunti ya Trans nzoia, maeneo ambayo yameripotiwa kuwa na maambukizi zaidi ya covid 19 wamekuwa wakiwasili katika soko hilo na kutangamana na wakazi bila kuzingatia kanuni za wizara ya afya hali inayo hatarisha afya yao.
Wametoa wito kwa uongozi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kuweka mikakati ya kudhibiti hali hiyo ili kuwalinda wakazi dhidi ya athari za janga la corona.