WAFANYIBIASHARA WA SARE ZA SHULE WALALAMIKIA KUPOKONYWA BIASHARA NA WAKUU WA SHULE.


Wafanyibiashara mjini Makutano katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameshutumu kile wamedai baadhi ya wakuu wa shule wameingilia biashara ya kuuza bidhaa shuleni hasa zile zinazotumika na wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza.
Wakiongozwa na naibu mwenyekiti wa chama cha wafanyibiashara chambers of commerce tawi la Pokot magharibi Mark Loriso wafanyibiashara hao wamesema biashara zao zimeathirika pakubwa kufuatia hali hiyo na licha ya lalama zao kwa idara husika hamna hatua ambazo zimechukuliwa.
Loriso sasa anatoa wito kwa mkuu wa elimu kaunti hii ya Pokot magharibi pamoja na waziri wa elimu prof. George Magoha kuingilia kati kukomesha biashara hiyo shuleni ili kuokoa biashara zao.
Hata hivyo mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wavulana ya Chewoyet moja ya shule zinazolaumiwa pakubwa Kiminisi Baraza amepinga vikali madai hayo akisema bidhaa hizo zinauzwa shuleni humo na baadhi ya wafanyibiashara mjini mkutano ambao wamepewa idhini na uongozi wa shule kufanya hivyo.