WAFANYIBIASHARA WA NGONO BUSIA WATAKA KUCHANJWA DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA


Wafanyibiashara wa ngono katika kaunti ya Busia wametoa wito kwa serikali kuwakumbuka na kuwapa chanjo dhidi ya virusi vya corona ikizingatiwa kwamba wanatangamana na watu wengi.
Wakiongozwa na Caroline Kemunto wafanyibiashara hao wamesema kuwa wanawahudumia wateja wengi kila siku hali ambayo inawakeka kwenye hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.
Wito wao unajiri wakati ambapo chanjo hiyo inatarajiwa kuanza kutolewa rasmi hapo kesho.