WAFANYIBIASHARA WA KACHELIBA WALALAMIKIA UBOVU WA BARABARA

Wakazi wa eneo la Kacheliba kaunti hii ya Pokot Magharibi wamelalamikia hali mbovu ya barabara ya kutoka Kacheliba hadi Nakuyen.
Wakiongozwa na Rhoda Sikamoi, wakazi hao ambao wengi wao ni wafanyibiashara wamesema kuwa inawachukua muda mrefu kufika sokoni ili kuendeleza shughuli zao huku wakitoa wito kwa uongozi wa eneo hilo kuikarabati barabara hiyo.
Aidha wakazi hao wanalalamika kuwa wanakadiria hasara baada ya bidhaa zao kuharibikia kwenye magari ambayo yanapata ugumu wa kupita barabara hiyo ambayo imeharibika kutokana na mvua kubwa inayoendelea kushuhudiwa kaunti hii.