WAFANYIBIASHARA MJINI KITALE WAKADIRIA HASARA KUTOKANA NA BARABARA BOVU.


Wakaazi wa miji mikuu kaunti ya Trans Nzoia pamoja na wafanyibiashara wamelalamikia ubovu wa barabara wakisema kwamba inaathiri biashara zao.
Wakizungumza na wanahabari wafanyibiashara hao wengi wao ambao wanafanyia shughuli zao mjini Kitale wamesema kuwa barabara nyingi mjini humo hazipitiki.
Juhudi za wafanyibiashara hao kurekebisha barabara hiyo kwa kuziba shimo imeambulia patupu.
Kauli ya wafanyibiashara hao imeungwa mkono na mbunge wa Saboti Caleb Amisi ambaye amesema kuwa kaunti ya Trans Nzoia haina cha kujivunia kwenye miaka 10 ya ugatuzi.