WAFANYIBIASHARA KONYAO WALALAMIKIA KUATHIRIWA NA WENZAO KUTOKA UGANDA.


Wafanyibiashara wa viazi kwenye soko la Konyao katika kaunti hii ya pokot magharibi wamelalamikia kuharibika bei ya bidhaa hiyo hali wanayoihusisha na viazi kutoka nchini Uganda.
Wakiongozwa Rosana kashior wafanyibiashara hao wamesema wenzao kutoka taifa hilo jirani wanaoleta bidhaa hiyo humu nchini wanauza kwa bei ya chini ikilinganishwa na ya humu nchini hali ambayo imeathiri pakubwa biashara yao.
Wametaka kuwekwe mikakati ya kuhakikisha kuwa bei ya bidhaa hiyo katika kaunti hii na inayotoka nchini Uganda inasawazishwa ili kuhakikisha hamna mfanyibiashara aneyeumia kutokana na utofauti katika bei ya viazi pande zote mbili.