WADAU WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUKABILI MIMBA ZA MAPEMA MIONGONI MWA WATOTO WA KIKE.

Na Benson Aswani
Ipo haja ya ushirikiano baina ya Wazazi, Serikali , walimu pamoja na wahisani katika kukabili swala la wasichana wadogo kupachikwa mimba za mapema jambo ambalo limechangia kuongezeka kwa idadi ya watoto wa kuranda randa mitaani.
Kwenye mkao na wanahabari baada ya kufungua rasmi bweni la wavulana pamoja na ukarabati lile la wasichana katika makao ya watoto ya children of hope Kenya eneo la Kitalale eneo bunge la Saboti kaunti kaunti ya Trans nzoia, mkurugenzi wa makao hayo Abraham Kiboki amesema ipo haja ya kutolewa kwa malezi bora mbali na ushauri nasaha kwa watoto ili kupunguza visa hivyo.
Kwa upande wake mwakilishi wadi ya Kinyoro Lawrence Mokosu ametaka serikali ya Kaunti ya Trans-Nzoia kupitia kwa wizara ya jinsia na ile ya elimu kutenga fedha maalum kwenye bajeti zao kusaidia watoto wasiojiweza katika makao yote ya watoto Kaunti ya Trans-Nzoia, ili kuwawezesha kupata makao, chakula, mavazi na hata elimu, akiongeza kuwa hii itasaidia kupunguza idadi ya watoto wa kurandaranda mitaani.