WADAU WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA ELIMU POKOT MAGHARIBI.

Wito umetolewa kwa wadau wa sekta ya elimu katika kaunti hii ya Pokot magharibi kushirikiana ili kuhakikisha kuwa viwango vya elimu vinaimarika hasa matokeo ya mitihani ya kitaifa.

Ni wito wake mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ambaye amesema kwamba kaunti hii itarejelea hali yake ya kufanya vyema katika mitihani hiyo iwapo tu kutakuwa na ushirikiano miongoni mwa wadau mbali mbali wakiwemo viongozi wazazi na walimu.

“kuna wakati pokot magharibi walikuwa wakifanya vizuri sana lakini wakafika mahali wakapotea kabisa. Ila naamini kwamba wadau tumejiandaa tunataka tuketi tushikane pamoja kwa maswala ya elimu ili turejeshe hadhi yetu kitaifa.” Alisema.

Amesema kwamba kwa muda wa miaka mitatu sasa shule zilizokuwa zikifahamika kwa kufanya vyema kwenye mitihani ya kitaifa kaunti hii hazijakuwa zikifanya vyema akisema kuwa uchunguzi unafaa kufaywa kubaini kiini cha hali hiyo.

“Hasa kwa miaka mitatu iliyopita hatujafanya vizuri na lazima tukubali. Zile shule kubwa kubwa za zamani sasa hazipo tena na tunataka kufahamu sababu ni nini.” Alisema.