WADAU WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUHIFADHI VYANZO VYA MAJI TRANS NZOIA


Siku ya ardhi duniani world earth day ikiadhimishwa leo,ipo haja ya kuimarisha juhudi za kukabili uharibifu wa vyanzo vya maji na chemichemi kama njia moja ya kuhifadhi na kuzuia kupotea kwa baadhi ya wanyama wanaoishi kwa kutegemea mazingira hayo.
Shirika moja la kimazingira linalopigania uhifadhi wa chemichemi lililoko kwenye mbunga ya wanyama ya kitaifa ya saiwa kaunti ya Trans nzoia kwa jina Kipsaina Cranes and Wetlands Conservation group likiongozwa na mwanzilishi Maurice Wanjala Sitiko limesema litatumia siku hii kuhamasisha jamii kupanda miti kwenye maeneo hayo ili kuzuia kupotea kwa swara aina ya Statunga, Ndege ya Koronga na tumbili aina ya Columbans.
Wakati uo huo Wanjala amesema kwa ushirikiano na washikadau wengine wa kupigania uhifadhi wa mazingira kaunti Trans-nzoia wanatazamia kupanda zaidi ya miche 50,000 kuadhimisha siku hii akiongeza kuwa wanalenga kupanda zaidi ya miche 200,000 msimu huu wa mvua.