WADAU WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUHIFADHI VYANZO VYA MAJI TRANS NZOIA.


Ipo haja ya ushirikiano baina ya serikali, wananchi na washikadau katika sekta ya mazingira ili kuhifadhi Chemichemi na vyazo vya maji katika Kaunti ya Trans-Nzoia.
Akihutubu kwenye maadhimisho ya siku ya Chemichemi duniani naibu mkurugenzi wizara ya Maji mazingira na mali hasili Nicholas Musonye amesema shughuli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na kilimo na ulishaji wa mifugo zimepelekea kudorora kwa sehemu hizo muhimu.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na Mwanzilishi wa kikundi cha Kipsaina Cranes and wetland conservation Maurice Wanjala akisema maeneo ya chemchemi yana umuhimu mkubwa kwa binadamu na makao kwa baadhi ya Wanyama.
Kwa upande wake Kaimu naibu kamishna kaunti ndogo ya Cherangani Fredrick Okwach amesisitiza haja ya kuhusisha umma katika uhifadhi wa chemchemi na vyanzo vya maji kwenye mto sinyereri na Chemichemi ya saiwa, akisema ina umuhimu mkubwa kwa wenyeji na serikali kutokana na mbuga ya kitaifa ya Saiwa.