WADAU WATAKIWA KUISAIDIA SHULE YA MSINGI YA KUTUNG BAADA YA BWENI KUTEKETEA.


Wadau mbali mbali katika kaunti hii ya Pokot Magharibi wametakiwa kujitokeza kuisaidia shule ya msingi ya Kutung eneo la Riwo baada ya bweni la shule hiyo pamoja na hifadhi ya chakula kuteketea na kusababisha hasara kubwa kwa wanafunzi na shule kwa jumla.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo David Simiyu hamna chochote kilichookolewa katika mkasa huo wa usiku wa kuamkia jana ambapo inakadiriwa mali ya takriban shilingi milioni 1.8 iliteketea.
Simiyu sasa anatoa wito kwa serikali ya kaunti hii, viongozi pamoja na mashirika yasiyo ya serikali kuisaidia shule hiyo kipindi hiki kwani amesema kuwa hawangeweza kuwatuma nyumbani wanafunzi kutokana na hali kuwa muhula wa kwanza unakaribia kutamatika.