WADAU WATAKIWA KUINGILIA KATI CHANGAMOTO ZINAZOKUMBA SHULE YA UPILI YA KIWAWA.


Wadau katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuingilia kati na kuisaidia shule ya upili ya wavulana ya Kiwawa iliyo katika eneo bunge la Kacheliba kufuatia changamoto nyingi zinazoikumba shule hiyo.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Luke Lotukoi amesema kwa sasa shule hiyo ina bweni moja pekee ambalo halitoshelezi idadi kubwa ya wanafunzi, madarasa machache pamoja na ukosefu wa ua hali ambayo inahatarisha usalama wa wanafuzi.
Aidha amesema kuwa shughuli nyingi katika shule hiyo zimelemazwa kutokana na uchache wa fedha, akiwahimiza wazazi kushirikiana na shule hiyo kupitia ulipaji wa karo ili kuwawezesha kuwahudumia wananfunzi inavyostahili.
Wakati uo huo Lotukoi amesema ujio wa janga la corona uliathiri masomo ya baadhi ya wanafunzi kwani baadhi hawajarejea shuleni kufikia sasa licha ya juhudi za uongozi wa shule hiyo kwa ushirikiano na machifu kuhakikisha kila mwanafunzi anarejea shuleni.