WADAU WATAKIWA KUCHANGIA JUHUDI ZA KUHAKIKISHA NIDHAMU MIONGONI MWA WANAFUNZI.


Wadau mbali mbali katika kaunti ya Pokot magharibi wametakiwa kuchangia juhudi za kuhakikisha nidhamu inadumishwa miongoni mwa vijana hasa wanafunzi.
Ni wito wake mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wavulana ya Holy Cross Kacheliba kaunti hii ya Pokot magharibi Stanley Pilakan ambaye amesema kuwa, utumizi wa mihadarati miongoni mwa vijana umechangia pakubwa utovu wa nidhamu, akitaka juhudi za pamoja ili kukabili swala hilo.
Wakati uo huo pilakan amesema shule hiyo ina idadi kubwa ya wanafunzi walio na mahitaji maalum , akitoa wito kwa wahisani zaidi kujitokeza na kuwasaidia wanafunzi hao, kwa kuwapa ufadhili ili pia wapate fursa ya kuendelea na masomo yao na kuafikia ndoto zao maishani.
Amesema shule hiyo ilifanya vyema katika mtihani wa kitaifa kwa kidato cha nne kcse kufuatia juhudi za walimu, na ushirikiano uliotolewa na wazazi kwa kuhakikisha wanafunzi wanasalia shuleni kupitia ulipaji wa karo kwa wakati.