WADAU WATAKIWA KUANGAZIA KWA KINA SWALA LA MATOKEO DUNI KATIKA MTIHANI WA KITAIFA KCSE POKOT MAGHARIBI.

Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio ni kiongozi wa hivi punde kuelezea kutoridhishwa na matokeo ya mtihani wa kitaifa kwa kidato cha nne KCSE katika kaunti hii.
Akizungumza na kituo hiki, Poghisio amesema kuwa shule ambazo zilitarajiwa kufanya vyema katika mtihani huo kaunti hii hazikuonekana popote.
Ametoa wito kwa wadau kuendesha uchunguzi kubaini chanzo cha matokeo hayo duni ambayo yamekuwa yakiripotiwa katika miaka ya hivi karibuni ili kuangazia jinsi ya kuyaimarisha katika miaka ijayo.
Poghisio amewataka viongozi wa kisiasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi kutoegemea zaidi maswala ya siasa na badala kushirikiana ili kuangazia jinsi ya kuimarisha viwango vya elimu.