WADAU WAPONGEZA HATUA YA KUDHINISHWA MJI WA KIMILILI KUWA MANISPAA.


Meneja wa manispaa ya mji wa Kimilili katika kaunti ya Bungoma John Ndombi amepongeza hatua ya mji huo kuidhinishwa katika gazeti rasmi la serikali kuwa manispaa.
Akizungumza afisini mwake Ndombi amesema kuwa hatua hiyo imepelekea mji huo kunufaika na miradi mbali mbali ikiwemo soko linalojengwa pamoja na barabara mbali mbali kwa ufadhili wa benki ya dunia pamoja na serikali ya kaunti hiyo ya bungoma.
Aidha Ndombi ameelezea imani kuwa hatua hiyo itapelekea wafadhili zaidi kujitokeza kufanikisha miradi katika mji huo hali ambayo itapelekea maendeleo zaidi na hata kuvutia wawekezaji katika siku za usoni.