WADAU WAHIMIZA KUREJESHWA KITENGO CHA NPR BONDE LA KERIO.


Kurejeshwa kwa kitengo cha polisi wa akiba NPR ndio suluhu ya kudumu kwa tatizo la utovu wa usalama kwenye eneo bunge la baringo kusini na vile vile kaunti ya baringo kwa jumla.
Ni kauli yake mwaniaji wa wadhifa wa uwakilishi wadi eneo la elchamus kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao 2022 kupitia chama cha kanu boniface lesaris.
Akiongea katika eneo la kapkiamo, kwenye eneo bunge la baringo kaskazini, lesaris amesema kuwa maafisa wa npr watasaidia pakubwa katika kuwakabili wezi wa mifugo ambao wamekuwa wakiwahangaisha wakazi kwa miaka nyingi.
Aidha lessaris amesema kuwa jamii fulani haifai kuangaziwa kama ya majangili ikizingatiwa kwamba ni watu wachache tu ndio wanaoendeleza wizi wa mifugo na uvamizi.
Kuhusu maswala ya uchaguzi lesaris amewataka viongozi wa kisiasa kuendesha kampeini zao kwa amani huku akiwashauri wananchi kuwachagua viongozi walio na ajenda zitakazowafaa.