WADAU WA MICHEZO TRANS NZOIA WAUNGA MKONO CBC.

Na Benson Aswani
Washikadau katika sekta ya michezo wanaunga mkono mtaala mpya wa CBC kwa kutilia maanani ukuzaji wa vipaji miongoni mwa wanafunzi shuleni badala ya kutegemea masomo ya nadharia pekee.
Akihutubu eneo bunge la Cherangani kwenye hafla ya kustaafu kwake, kiongozi wa shirika la michezo Trans-Nzoia Youths Sports Association (TYSA) Francis Gishuki amesema ipo haja kwa washikadau kuja pamoja na kuweza kushawishi mitazamo na sera ya kutumia michezo katika kubadili maisha ya vijana humu nchini, swala ambalo amesema amekuwa alipigania kwa miaka 25 alipokuwa kwenye usakani wa shirika hilo.
kwa upande wake Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la TYSA Carol Ndalila amesema uongozi wake unalenga kuendeleza ukuzaji na vipaji miongoni mwa vijana haswa wale wa kike mbali na kukuza uongozi miongoni mwa akina mama.