WADAU WA ELIMU WATAKIWA KUWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA ELIMU POKOT MAGHARIBI.
Mbunge wa Kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Moroto ametoa wito kwa wadau wa elimu kaunti hii kuweka mikakati mwafaka itakayohakikisha sekta ya elimu inaimarika zaidi.
Moroto amesema matokeo duni ambayo yalirekodiwa katika mitihani ya kitaifa mwaka jana katika kaunti hii yalichangiwa na mikakati duni hasa uwepo na kamati za shule ambazo zimebuniwa kutokana na misukumo ya kisiasa.
Wakati uo huo Moroto amewataka wakuu wa elimu pamoja na wakuu wa shule kaunti hii kuimarisha juhudi zao na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kitaaluma bila kuzingatia miegemeo ya kikabila ili kuboresha viwango vya elimu.