WADAU TRANS NZOIA WASHINIKIZA KUTAMBULIWA HAKI ZA WANAUME NCHINI.
Ipo haja ya kuwasilishwa kwa muswada na kubuniwa kwa sheria mpya bungeni itakayotoa nafasi ya kulindwa kwa haki za wanaume nchini, kutokana na kuwepo sheria zinazowalinda akina mama na watoto na kuwasahau wanaume.
Kwa mujibu wa wakili na mchanganuzi wa maswala ya sheria na kikatiba kutoka Kitale kaunti ya Trans nzoia Walter Wanyonyi, sheria za humu nchini zimembagua mwanamume, ikizingatiwa serikali na mashirika yasio ya kiserikali yametilia mkazo kutetea haki za akina mama na watoto na kuwaacha nje wanaume wengi wanaodhulumiwa katika jamii, jambo ambalo limepelekea kuongezeka kwa visa vya mauaji miongoni mwa jamii.
Wakati huo huo Wakili Wanyonyi ametoa wito kwa Wabunge wa kitaifa kuwasilisha bungeni sheria zitakazo leta usawa miongoni mwa wanaume, wanawake, na watoto bila ya ubaguzi unaoshuhudiwa kwa sasa, mbali na kupasisha hoja ya kubuniwa kwa kitengo maalum kwenye vituo vya polisi vitakayoushughulikia dhuluma dhidi ya wanaume.