WADAU POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA VIWANGO VYA ELIMU.


Ipo haja ya wadau katika sekta ya elimu kaunti hii ya Pokot magharibi kuweka mikakati ya jinsi ya kuimarisha matokeo katika mitihani ya kitaifa kwenye kaunti hii.
Akizungumza katika hafla ya ukumbusho wa mwanzilishi wa kanisa la mafuta pole dini ya roho Afrika kaunti hii ya Pokot magharibi, aliyekuwa gavana wa kaunti hii Simon Kachapin amesema kuwa shule nyingi katika kaunti hii hazikufanya vyema katika mtihani wa mwaka 2021 kulingana na matokeo yaliyotangazwa na waziri wa elimu Prof. George Magoha.
Kachapin ambaye ambaye pia ametangaza nia ya kuwania tena kiti cha ugavana katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti amesema viongozi katika kaunti hii wametelekeza pakubwa sekta ya elimu, huku pia akilaumu uhamisho wa walimu wa kaunti hii kuhudumu katika kaunti nyingine kuwa chanzo cgha matokeo duni katika mitihani hiyo.
Ni kauli ambayo imetiliwa mkazo na mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ambaye amesema iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kushughulikia hali hiyo huenda kaunti hii ikakosa kupata wanafunzi ambao wanasomea kozi zenye ushawishi hali ambayo huenda ikaifanya kutokuwa katika viwango sawa na kaunti zingine.