WADAU KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAENDELEA KUPIGIA DEBE MFUMO MPYA WA CBC.
Na Benson Aswani
Baadhi ya wadau katika sekta ya elimu kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kupigia debe mfumo mpya wa elimu CBC wanaosema kuwa ni bora zaidi ikilinganishwa na mfumo wa awali wa 8.4.4.
Malimu mkuu wa shule ya upili ya Chewoyet Samwel Kiminisi Barasa amesema kuwa mfumo huu ndio utatatua tatizo kubwa ambalo linawakabili wananchi la ukosefu wa ajira kwani CBC itawawezesha vijana kujiajiri na kutotegemea kuajiriwa punde wanapomaliza masomo yao.
Kiminisi ametoa wito kwa wadau kuunga mkono serikali ili kufanikisha utekelezwaji wa mfumo huo kwa manufaa ya vijana nchini.
Ikumbukwe mfumo huo umekuwa ukipokea pingamizi kutoka kwa baadhi ya wadau ambao wamesema ni ghali mno kwa wazazi huku kesi ikiwasilishwa mahakamani kupinga utekelezwaji wa mfumo wenyewe.