WADAU KATIKA SEKTA YA ELIMU WATAKA USALAMA KUIMARISHWA KATIKA MASHULE ZA MIPAKANI

Wadau wa sekta ya elimu katika kaunti ya elgeiyo marakwet sasa wanaitaka serikali kuu kuwahakikishia usalama wao walimu wanaofunza kwenye shule zilizoko eneo la bonde la kerio.
Katibu mkuu wa chama cha kitaifa cha walimu knut kaunti hiyo john cheberir amesema kuwa walimu katika eneo hilo kwa sasa wanaishi kwa wasi wasi baada ya wenzao wawili kuuwawa na wezi wa mifugo ndani ya katika kipindi cha siku mbili.
Akiongea na wanahabari cheberii aidha amependekeza walimu kupewa nafasi ya kufunza kwenye shule zilizo karibu na wanakoishi au kutengewa makazi kwenye shule wanazofunza iwapo watalazimika kufanya kazi mbali na makwao.
Naye katibu wa chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri kuppet kwenye kaunti hiyo paul biwot , amesema kuwa chama hicho hakitawaruhusu wanachama wake kuhudumu kwenye maeneo yasiyokua na usalama wa kutosha.