WADAU KATIKA SEKTA YA ELIMU WASHAURIWA KUWEKA MIKAKATI MAHUSUSI YA KUSITISHA MIGOMO YA WANAFUNZI


Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa ametoa wito kwa wadau katika sekta ya elimu kuweka mikakati mahususi ya kuzungumza na wanafunzi ili kutatua maswala yanayowathiri kuzuia misururu ya migomo inayoshuhudiwa katika shule tofauti za humu nchini.
Akiongea na wanahabari Barasa amesema kuwa maswala ambayo wanafunzi wanatoa yanaweza kuangaziwa mapema akisema walimu hawastahili kupuzilia mbali wanafunzi hao.
Kwa upande wa kisiasa mbunge huyo amesema kuwa wakaazi katika maeneo bunge ya Kabuchai na Matungu wanastahili kupewa fursa kuchagua kiongozi bora bila ya kushinikizwa kwa msingi wa vyama vya kisiasa.