WADAU KATIKA SEKTA YA ELIMU ENEO LA SWAM WAPONGEZWA KWA MATOKEO BORA.


Wadau katika sekta ya elimu eneo la Swam kaunti ya Pokot magharibi wamepongezwa kwa juhudi ambazo zilipelekea shule za eneo hilo kufanya vyema katika mtihani wa KCSE ambao matokeo yake yalitangazwa mapema juma lililopita.
Mwakilishi wadi wa eneo hilo Robaret Komole aidha ametoa wito kwa wadau hao kufanya juhudi zaidi ili kuhakikisha wanafunzi wa shule hizo wanafanya vyema zaidi katika mitihani ya miaka ijayo.
Aidha Komole ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya elimu katika bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi amesema kwa jumla shule za kaunti hii zilifanya vyema katika mtihani huo licha ya changamoto ambazo zilisababishwa na janga la corona.