WABUNGE WATAKIWA KUTENGA FEDHA ZA KUFADHILI WANAFUNZI KUTOKA JAMII MASIKINI.


Mwakilishi wadi wa Keiyo ambaye pia ni kinara wa wachache katika bunge la kaunti ya Trans-nzoia Emmanuel Waswa ametaka wabunge wa kitaifa kutenga fedha zaidi katika fedgha za ustawishaji maeneo bunge (NGCDF) kwa minajili ya kufadhili wanafunzi kutoka jamii maskini.
Akihutubu eneo la Kolongolo Waswa amesema kutokana makali ya covid 19 na sheria za kutotoka nje kuanzia saa moja usiku iliyowekwa kwa kaunti 13 za maeneo ya magharibi na nyanza itaadhiri pakubwa wazazi kupata karo ya wanafunzi wao wanapojiunga na shule za upili na vyuo vikuu.
Wakati huo huo Waswa amewataka wabunge wa kitaifa pia kubuni sheria zitakazo saidia usawa wa kuajiriwa kwa walimu katika shule za mashinani kwani shule nyingi nchini za umma zinashuhudia upungufu wa mkubwa walimu haswa katika shule za upili.