WABUNGE WA FORD KENYA WAAPA KUPITISHA MSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA VYAMA.

NA BENSON ASWANI
Wabunge wanaoegemea chama cha Ford Kenya katika kaunti ya Trans nzoia wameapa kuhakikisha kuwa mswada wa marekebisho ya sheria za vyama unapitishwa vikao vya bunge kuendelea kujadili mswada huo vinapotarajiwa kurejelewa hiyo kesho jumatano na ijumaa.
Wakiongozwa na mbunge wa Kiminini Dkt Chris Wamalwa, viongozi hao wamesema kuwa hatua hii itasaidia kumaliza mizozo katika vyama vya kisiasa ambavyo vinaunda miungano kwa kutoa nafasi kwa ugavi sawa wa fedha zinazotolewa kwa vyama hivyo.
Aidha Wamalwa ametumia fursa hiyo kushutumu chama cha ODM kwa kile amedai kuwa kimedinda kutoa mgao wa fedha kwa vyama tanzu vya uliokuwa muungano wa NASA uliojumuisha vyama vya ODM, Wiper, ANC, Ford Kenya na chama cha mashinani CCM licha fedha hizo kutolewa na msajili wa vyama vya kisiasa.