WAATHIRIWA WA KIFUA KIKUU WATAKIWA KUFANYA VIPIMO VYA KILA MARA.
Wito umetolewa kwa wakenya kufanya mazoea kufika katika vituo vya afya ili kupimwa kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu.
Ni wito ambao umetolewa na mtaalam wa magonjwa ya mapafu katika hospitali ya Kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi Dr. Jackson Lomuk ambaye amesema kuwa ugonjwa wa kifua kikuu una tiba iwapo utagunduliwa mapema na mwathiriwa kuzingatia ushauri unaostahili.
Lomuk amesema ugonjwa huu umekuwa sugu miongoni mwa baadhi ya wakazi kutokana na hali kuwa wamesusia kufika katika vituo vya afya ili kupimwa na kubadilishiwa dawa wanapogundulika kuwa nao.
Amesema kuwa mtindo wa maisha ya watu wengi ikiwemo kutumia bidhaa zinazotokana na tumbaku, unywaji pombe, ulaji wa nyama kiholela pamoja na kutozingatia lishe bora kumepekea kukithiri magonjwa ya kifua kikuu pamoja na saratani.