WAAKILISHI WADI BUNGOMA WATAKIWA KUSITISHA MIPANGO YA KUMBANDUA GAVANA WANGAMATI
Viongozi wa dini katika kaunti ya Bungoma wametoa wito kwa waakilishi wadi katika kaunti hiyo kufanya mazungumzo na gavana wao Wyclife Wangamati ili kutatua uhasama uliopo kuhusu mchakato wa kuataka kumwondoa afisini.
Wakiongozwa na kasisi wa kanisa la Evanjelical ministries mjini Chwele Ben Mulupi viongozi hao wamesema mazungumzo kati ya waakilishi wadi na gavana huyo yatamaliza utata uliopo na kutoa nafasi ya kuimarisha utendakazi wa serikali ya kaunti ya Bungoma.
Wakati uo huo viongozi hao wamewashauri vijana kutotumiwa vibaya na wanasiasa taifa linapoelekea kwenye siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 ambao ni mwaka ujao.
Aidha wametoa wito kwa viongozi katika jamii kushirikiana na kanisa katika kuweka malezi bora kwa vijana kwa lengo la kuboresha maisha yao.