WAAJIRI WATAKIWA KUWATENGEA KINA MAMA WANAONYONYESHA NAFASI YA KUWANYONYOSHA WANAO.


Takwimu zinaonyesha kwamba 2/3 ya akina Mama wanaonyonyesha wanao wameajiriwa na serikali na katika sekta mbalimbali ya kibinafsi nchini, hivyo ipo haja ya hamasisho kwa waajiri na jamii kuwatengea akina Mama hao muda na chumba maalum cha kuwanyonyesha wanao na baada ya kurejea kazini wanapokamilisha likizo ya miezi mitatu ya kujifungua.
Akiwahutubia wanahabari msimamizi wa maswala ya lishebora Kaunti ya Trans-Nzoia Lydia Kimani amesema hatua hiyo itasaidia kuafikiwa mwongozo wa WHO na wizara ya afya unaohitaji mtoto kunyonya maziwa ya mama kwa takriban miezi sita bila ya kuongeza chakula chochote.
Aidha Bi Kimani amesema maziwa ya Mama yana umuhimu mkubwa kwa mtoto mchanga , kwani utafiti unaonyesha kuwa kunyonyeshwa kwa mtoto kwa njia ipasavyo kunaweza kupunguza maambukizi pamoja na vifo miongoni mwa watoto haswa maradhi ya kuendesha ambayo husababisha vifo vingi miongoni mwa watoto na pia kumuepusha Mama dhidi ya saratani ya matiti na ile ya utumbo wa uzazi au “overian cancer”.
Wakti huo huo Bi Kimani ameongeza kuwa mpango wa friendly work place breast feeding utaleta manufaa mengi kwa waajiri mbali na kuongeza bidii ya mama kazini,akipendekeza kubuniwa kwa mwongozo mwafaka utakaowalinda kina mama wanaonyonyesha ikiwa ni pamoja na kuzingatia mahitaji yao kazini.