WAAJIRI TRANS NZOIA WASUSIA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYIKAZI DUNIANI.

Viongozi wa wafanyakazi katika Kaunti ya Trans Nzoia wamelalamikia hatua ya waajiri kutofika kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyikazi duniani na kusikia malalamishi ya wafanyakazi wao.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa wafanyakazi wa serikali ya Kaunti Samuel Kiboi, viongozi hao wamesikitikia hatua hiyo wakisema ni sharti kila mwajiri kutilia maanani matakwa ya wafanyakazi nchini.
Ni matamshi yaliyoungwa mkono na Mwenyekiti wa mabawabu Kenya National private security workers Union Chrisantus Wamalabe akisema ipo haja ya ushirikiano wa muungano wa wafanyakazi na waajiri wa wafanyakazi hao ili kuafikiwa kwa utoaji huduma bora na wa hali ya juu, pia akilalamikia malipo duni kwa wafanyakazi.
Katibu wa muungano wa KUBEA Wilfred Olando amehimiza wafanyakazi kujiunga katika miungano ya wafanyakazi ili kupata fursa ya kupigania haki zao mbali na matakwa yao kuzingatiwa kwa mujibu wa sheria.