VYAMA VYA ANC, KANU ,WIPER NA FORD KENYA CHA ZINDUA MUUNGANO WA ONE KENYA ALLIANCE


muungano wa one kenya alliance umezindua mpango wa kufanya ziara kote nchini ili kuwahamasisha wakenya kuhusu utangamano.
hata hivyo muungano huo ambao unahusisha vyama vya anc, ford kenya, wiper na kanu umesema ziara hizo zitaanza baada ya kupungua maambukizi ya virusi vya corona.
muungano huo umesisitiza kuwa unaunga mkono mpango mzima wa bbi ukisema una manufaa makubwa kwa wakenya.
Moses Wetanguala wa chama cha ford Kenya amesifia muungano huku mwenyekiti wa chama cha Kanu Gideon Moi amesema lengo kuu la muungano huo ni kukomesha siasa za ukabila ambazo amesema zimepitwa na wakati kauli ambayo imesisitizwa na kinara wa ANC Musalia Mudavadi.