VIWANGO VYA MAAMBUKIZI YA CORONA VYARIPOTIWA KUPANDA POKOT MAGHARIBI.


Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuendelea kuzingatia kanuni za wizara ya afya kuzuia msambao wa virusi vya corona ili kusalia salama hasa msimu huu ambapo maambukizi yanaripotiwa kuongezeka nchini.
Afisa katika wizara ya afya kaunti hii Julia Sipoti amesema kuwa viwango vya maambukizi vimeripotiwa kuongezeka katika kaunti hii ya pokot magharibi hasa baada ya sherehe za mwezi desemba ambapo watu wengi walitangamana bila kuzingatia kanuni za kukabili maambukizi.
Sipoti amewataka wakazi ambao hawajapokea chanjo dhidi ya covid 19 kufika katika vituo vya afya kupokea chanjo hiyo huku pia akitumia fursa hiyo kuwaarifu wale ambao wamepokea chanjo hiyo kufika ili kupokea chanjo ya ziada ili kuhakikisha kinga kamilifu.