VITUO ZAIDI VYA KUTOA CHANJO YA COVID 19 KAUNTI YA BUNGOMA VIMEFUNGULIWA


Mshirikishi wa maswala ya magonjwa ibuka kwenye kaunti ya Bungoma Moses Wambusi amesema kuwa vituo 20 vya kutoa chanjo ya covid 19 vimefunguliwa kwenye maeneo bunge yote 10 kwenye kaunti ya Bungumo ili kuwafaa wenyeji.
Akizungumza kwenye mkutano uliowaleta pamoja wadau mbali mbali kweye kaunti hiuo, Wambusi amesema kuwa madaktari ambao watahusika kutoa chanjo hiyo tayari wameanza kupokea mafunzo.
Shughuli ya utoaji wa chanjo hiyo inatarajiwa kung’oa nanga rasmi siku ya ijumaa wiki hii.