VITENGO VYA USALAMA VYATAKIWA KUWA MAKINI MIPAKANI PA POKOT MAGHARIBI.


Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amewataka wadau katika sekta ya usalama kuwa makini na kudumisha usalama katika mipaka ya kaunti hii ya pokot magharibi na kaunti jirani hasa ile ya Elgeyo marakwet.
Poghisio amesema kuwa huenda wahalifu wakatumia fursa hii ambapo wakazi maeneo hayo wanaendelea na harakati za kusherehekea msimu wa krismasi na mwaka mpya kutekeleza uhalifu hasa maeneo ya Chesogon.
Wakati uo huo Poghisio amewataka wakazi wa maeneo haya kudumisha amani na kujitenga na visa vya wizi wa mifugo anavyosema kuwa vimesababisha kaunti zinazopatikana katika bode la kerio kusalia nyuma zaidi kimaendeleo.