VISA VYA UVAMIZI VYARIPOTIWA KUPUNGUA MPAKANI PA POKOT MAGHARIBI NA TURKANA.


Chifu wa eneo la songok, ombolion eneo bunge la pokot kaskazini kaunti hii ya pokot magharibi Joseph Korkimul amepongeza juhudi za amani ambazo zinaendelezwa eneo hilo la mpakani baina ya kaunti hii ya pokot magharibi na kaunti jirani ya Turkana.
Korkimul amesema kuwa licha ya kushuhudiwa visa vichache vya wizi wa mifugo wakazi wa maeneo hayo ambayo yalishuhudia visa vya uvamizi wa kila mara katika miaka ya awali wanafanya juhudi za kuhakikisha kuwa kunaafikiwa amani.
Aidha Korkimul ametoa wito kwa serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa utulivu unaendelea kushuhudiwa eneo hilo ili kuwapa wanafunzi fursa ya kuhudhuria masomo na pia kuruhusu shughuli nyingine za maendeleo.