VISA VYA UKEKETAJI VYENDELEA KURIPOTIWA POKOT MAGHARIBI.


Licha ya juhudi za serikali na mashirika mbalimbali ya kijamii kaunti hii ya Pokot magharibi kukabili visa vya ukeketaji imebainika kwamba visa hivyo vinaendelezwa kisiri.
Hii ni baada ya mama mmoja mkazi wa eneo la mosop kaunti hii kudaiwa kulazimishwa na mmewe pamoja na mama mkwe kukeketwa kisa ambacho kimeshutumiwa vikali na mashirika ya kijamii kaunti hii ya Pokot magharibi.
Afisa katika wakfu wa IREB foundation Domtila Chesang amewapongeza chifu wa eneo hilo na naibu wake kwa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha washukiwa wanakamatwa.
Wakati uo huo Domtila amelalamikia ongezeko la visa vya dhuluma za jinsia ambazo zinaendelezwa na jamii dhidi ya watoto akielezea haja ya jamii hasa wazazi kutekeleza majukumu yao ya kuhakikisha usalama wa wanao ili kukabili visa hivi.