VISA VYA UKEKETAJI VIMEPUNGUA KWA ASILIMIA KUBWA KATIKA ENEO LA KACHELIBA KAUNTI HII YA POKOT MAGHARIBI


Na Benson Aswani
Shughuli ya kutoa uhamasisho kwa umma kuhusu athari za ukeketaji imepelekea kupungua pakubwa visa hivyo eneo lake Kapchok katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Haya ni kulingana na chifu wa eneo hilo Philip Wapale ambaye aidha amesema kupungua kwa visa hivyo pia kumechangiwa na ushirikiano na maafisa kutoka taifa jirani la Uganda ambao wamekuwa wakizuia wanaojaribu kutorokea wilaya ya Amudat kuendeleza visa hivyo.
Hata hivyo Wapale amesema kuwa kipindi kirefu ambacho wanafunzi walisalia nyumbani baada ya kufungwa shule kufuatia janga la corona kilipelekea wanafunzi wengi wa kike kupata mimba za mapema kufuatia kushiriki ngono za kiholela hali iliyopelekea wengi wao kuachia masomo njiani.
ameendelea kuwahimiza wanafunzi kike ambao walipata mimba za mapema na kujifungua kurejelea masomo ili kutimiza ndoto zao maishani hasa baada ya serikali kushinikiza hilo.