VISA VYA MIMBA MIONGONI MWA WATAHINIWA WA KIKE VYAENDELEA KURIPOTIWA.

Jumla ya watahiniwa 87 walipachikwa mimba katika Kaunti ya Pokot Magharibi.

Kulingana na wizara ya Elimu Kaunti ya Pokot Magharibi, darasa la nane linaongoza kwa idadi ya waliopachikwa mimba ikiwa ni 46, kidato cha nne ni 81 huku waliopachikwa mimba kwenye gredi ya sita wakiwa kumi. 

Eneo la Kipkomo linaongoza kwa jumla ya watahiniwa 26 wanaofanya mtihani wakiwa wajawazito, Pokot ya kati 17, Pokot Kusini 16, Kacheliba 14 sawa na Kapenguria iliyo na watahiniwa 14 wenye uja uzito.

Hata hivyo hakuna mtahiniwa ambaye ameripotiwa kujifungua au kupata tatizo la maumivu wakati wa mitihani inayoendelea.

Katika kaunti ya narok jumla ya watahiniwa wa kike 248 wanafanya mitihani wakiwa na mimba.

Ikumbukwe hii ni mara ya kwanza kwa wa  taifa kuandaa mitihani tatu ya kitaifa tangu kuzinduliwa mtaala mpya wa elimu CBC.

Watahiniwa wa gredi ya sita wanafanya mtihani wao wa kitaifa KPSEA huku jopo lililobuniwa na rais William Ruto kutathmini utekelezwaji mtaala huo likitarajiwa kutoa ripoti yake baada ya kuandaa vikao vya kutafuta maoni kutoka kwa wananchi kote nchini kuhusu mtaala huo.

Hatua hii ilichukuliwa na rais Ruto kufuatia malalamishi kutoka kwa baadhi ya wazazi ambao walitaka mtaala huo kusitishwa kufuatia kile walisema ni ghali mno.

Hata hivyo rais Rais Ruto alisema kwamba serikali yake haina nia ya kuufutilia mbali mtaala huo ila kuufanyia tu marekebisho.

Aliyekuwa waziri wa elimu katika serikali ya rais mustaafu Uhuru Kenyatta, George Magoha alitoa wito kwa waziri wa elimu wa sasa kutofutilia mbali mtaala huo akiuataja kuwa wenye manufaa makubwa kwa wanafunzi ikilinganishwa na mtaala wa 8.4.4.