VISA VYA KUJIFUNGUA WATAHINIWA KATIKA MITIHANI LATARAJIWA KUPUNGUA MWAKA HUU.


Swala la watahiniwa wa kike kufanya mitihani ya kitaifa wakiwa wajawazito linatarajiwa kupungua pakubwa kwenye baadhi ya shule katika kaunti hii ya pokot magharibi mwaka huu ikilinganishwa na jinsi ilivyoshuhudiwa katika mitihani ya mwaka jana.
Mwalimu mkuu wa shule ya wasichana ya St Bakhita Grace Kakuko amesema kuwa hali hii imetokana na mikakati mwafaka iliyowekwa kwa ushirikiano na wadau mbali mbali kaunti hii ikiwemo afisi ya naibu kamishina, machifu pamoja na wazazi.
Kakuko amesema kuwa miongoni mwa mikakati ambayo imechangia hali hiyo ni pamoja na kuwashauri wanafunzi mara kwa mara kuhusu athari za kujihusisha na ngono za mapema, kuwahusisha kikamilifu wazazi pamoja na hatua ya idara ya usalama kupiga marufuku sherehe za usiku.