VIONGOZI ZAIDI WAPINGA UWEZEKANO WA KUAHIRISHA UCHAGUZI MKUU UJAO.
Hisia mseto zimeendelea kuibuliwa nchini kufuatia shinikizo kutoka kwa baadhi wa viongozi kutaka uchaguzi mkuu wa mwaka ujao wa 2022 kuahirishwa ili kutoa fursa ya kufanyia katiba marekebisho kupitia mpango wa upatanishi BBI.
Wa hivi punde kuzungumzia swala hilo ni mbunge wa Kacheliba kaunti hii ya Pokot magharibi Mark Lumnokol ambaye amepinga vikali shinikizo hizo akisema kuwa taifa la Kenya linatawaliwa na sheria na ni sharti sheria za nchi kufuatwa kuhusu tarehe ya uchaguzi mkuu.
Lumnokol amesema kuwa viongozi wanaoshinikiza kuahirishwa uchaguzi huo wana malengo yao ya kibinafsi akiwataka wakenya kupuuzilia mbali shinikizo hizo na kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi huo utakaoandaliwa mwezi Agosti mwaka ujao.