VIONGOZI WATAKIWA KUZINGATIA UWAZI KATIKA MAJUKUMU YAO POKOT MAGHARIBI.


Viongozi wa kisiasa katika kaunti hii ya pokot magharibi wametakiwa kutekeleza majukumu yao waliyopewa na wananchi kikamilifu kwa kuzingatia uwazi katika shughuli zote wanazotekeleza.
Ni wito wake spika wa bunge la kaunti hii ya pokot magharibi Catherine Mukenyang ambaye amesema kuwa kiongozi yeyote anayehudumu katika wadhifa wa umma alipewa nafasi hiyo ili kutoa huduma bora kwa mwananchi wala si kuitumia kujinufaisha kwa njia zisizostahili.
Wakati uo huo mukenyang ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii ya pokot magharibi kuwa makini na viongozi wanaowachagua nyakati za uchaguzi ili kuhakikisha kuwa wanawachagua viongozi ambao watawahudumia kwa kuzingatia uwazi.