VIONGOZI WATAKIWA KUZINGATIA UMOJA BAADA YA BBI.


Baada ya mahakama ya rufaa kusitisha mchakato mzima wa BBI Viongozi nchini wametakiwa kuzingatia umoja wa kitaifa huku uchaguzi mkuu wa mwaka ujao ukikaribia.
Rais wa bunge la vijana nchini ambaye pia ni mwaniaji kiti cha mwakilishi wadi ya mnagei kaunti hii ya Pokot magharibi Richard Todosia amesema kuwa japo baadhi ya mapendekezo kwenye BBI yalikuwa mazuri ni sharti viongozi husika watumie njia inayokubalika kisheria kuyaidhinisha badala ya kulazimisha kura ya maamuzi inayoweza kuwagawanya wakenya.
Wakati uo huo Todosia ameitaka wizara ya afya kusambaza chanjo ya virusi vya corona kwa wingi ili wakenya wanaojitokeza kupokea chanjo hiyo waweze kushugulikiwa ili Kenya iwe salama na uchumi uweze kufunguliwa.