VIONGOZI WATAKIWA KUWASAIDIA WANAFUNZI WENYE MATATIZO YA KARO BARINGO.
Katibu wa kitaifa wa idara ya elimu ya juu katika chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET Sammy Chelang’a ameirai jamii na viongozi kuwasadia wanafunzi wanaokumbwa na tatizo la ulipaji wa karo.
Akiongea mjini kabartonjo kwenye eneo bunge la baringo kaskazini kaunti ya Baringo, chelang’a amesema kuwa baadhi ya wanafunzi bado hawajaripoti shuleni ikiwa ni siku ya tano baada ya shule kufunguliwa kwa muhula wa tatu kutokana na ukosefu wa fedha za kulipia karo.
Aidha chelang’a ambaye ametangaza nia ya kugombea wadhifa wa ubunge eneo hilo amewarai walimu wakuu kutowatuma nyumbani wanafunzi karo na badala yake wafanye mazungumzo na kuafikiana na wazazi jinsi watakavyolipa karo ya wanao.