VIONGOZI WATAKIWA KUSITISHA MIVUTANO POKOT MAGHARIBI.

Na Benson Aswani

Wito umetolewa kwa viongozi wa kisiasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi kusitisha mivutano ya mara kwa mara na badala yake kutumia muda wao mwingi kuwapa wakazi huduma zinazostahili.
Mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto amesema kuwa huduma nyingi muhimu ambazo zinapasa kutolewa kwa wananchi zimetelekezwa kutokana na mivutano ya mara kwa mara isiyo muhimu miongoni mwa viongozi katika kaunti hii.
Aidha Moroto amewataka viongozi kutowawekea vikwazo wanasiasa wenzao wanaopania kugombea nyadhifa za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao na kuwapa fursa wananchi kutekeleza haki yao ya kikatiba kuwachagua viuongozi wanaowapendelea.

WhatsApp us