VIONGOZI WATAKIWA KUKUMBATIA UAMUZI WA MAHAKAMA KUHUSU BBI.


Mahakama ya rufaa ikitarajiwa leo kutoa uamuzi kuhusu mchakato wa kufanyia katiba marekebisho kupitia mpango wa BBI miito imeendelea kutolewa kwa viongozi wa kisiasa kukubali matokeo ya kesi hiyo.
Wakiongozwa na Henry Ngata, wakazi wa makutano kaunti hii ya pokot magharibi wamewataka viongozi kukubaliana na uamuzi huo na kutoelekea mahakani kuwasilisha rufaa kwani taifa linastahili kusonga mbele hasa wakati huu ambapo imesalia chini ya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Aidha wakazi hao wametoa wito kwa majaji wa mahakama hiyo kutotoa uamuzi ambao umeshawishiwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na badala yake kuzingatia mustakabali wa taifa kwani matumaini ya wakenya yako kwenye mahakama hiyo.