VIONGOZI WATAKIWA KUINGILIA KATI NA KUTATUA SUALA LA UTOVU WA USALAMA MIPAKANI.
Wakaazi wa kaunti ya pokot magharibi wanalalamikia wanachokitaja kama ulegevu wa viongozi wa taifa na wa kaunti zinazoathirika na ukosefu wa usalama katika kutafuta suluhu ya tatizo hilo katika bonde la ufa
Kwa muda sasa , kaunti za pokot magharibi, turkana , baringo na elgeyo marakwet zimeshuhudia utovu wa usalama kwa mashambulizi ya mara kwa mara zinazoambatana na wizi wa mifugo na vifo vya wakaazi
Matukio hayo yamewaacha wakaazi na maswali mengi, wengi wakionyesha kukerwa na viongozi wanaotoka kaunti husika kuendelea na siasa kama kawaida badala ya kutafuta suluhu ya kudumu ya tatizo hilo
Aidha wakaazi wa kaunti ya pokot magharibi wameirai serikalikuchukuwa hatua mwafaka kutatua tatizo hili