VIONGOZI WASHAURIWA KUDUMISHA AMANI WAKATI HUU WA KAMPEINI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI
Baadhi ya wakazi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameelezea kughadhabishwa na kile wamedai hatua ya viongozi wa kaunti hii kuegemea siasa pakubwa na kutelekeza miradi ya maendeleo ya kuwanufaisha wananchi.
Wakiongozwa na Elina Kamarich mkazi wa Mathare viunga vya mji wa makutano, wakazi hao wameshutumu viongozi kwa kufeli kutekeleza miradi ambayo waliahidi wakati wakiendeleza kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.
Wakati uo huo wakazi hao wamewataka wanasiasa kuendesha kampeni za amani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi agosti na kukoma kutumia vijana kuzua vurugu kwa manufaa yao ya kisiasa.