VIONGOZI WANDELEA KULALAMIKI UTOVU WA USALAMA POKOT MAGHARIBI.

NA BENSON ASWANI
Viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kulalamikia visa vya utovu wa usalama mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet hasa eneo la Cheptulel, ambapo wakazi wa kaunti hii ndio waathiriwa wakuu wa visa hivyo.
Akizungumza na kituo hiki seneta wa kaunti hii Samwel Poghisio amesema kuwa wakazi wa kaunti hii wametelekezwa kwa swala zima la usalama kufuatia hatua kuwa maafisa wa akiba NPR kutoka upande wa Elgeyo marakwet wamepewa bunduki hali wenzao wa pokot magharibi hawana silaha hizo.
Poghisio ameitaka serikali kujenga kambi ya maafisa wa polisi eneo hilo la mpakani jinsi ilivyofanya katika kaunti ya Elgeyo marakwet na kuwapa mafunzo ya kutosha maafisa wa akiba NPR pamoja na kuwakabidhi bunduki ili kuwalinda wakazi dhidi ya wavamizi.
Aidha Poghiso amewataka wakazi wa kaunti hii kuendelea kudumisha amani wakati viongozi wakiendelea kuishinikiza serikali kuhakikisha kuwa suluhu ya kudumu inapatikana na kutia kikomo kwa visa vya kuuliwa wakazi kiholela.