VIONGOZI WAMETAKIWA KUINGILIA KATI NA KUTATUA SUALA LINALOWAKUMBA WENYEJI WA KOSIKE KULE LOROO UGANDA WANAHOFU YA KUNYAKULIWA MASHAMBA


Viongozi katika kijiji cha kosike kule LOROO , Uganda wamefanya mkutano uliopangwa na kikundi cha kanisa la katholiki almaarufu Catholic Land Desk kinachojulikana kwa kuhusika pakubwa katika kutatua maswala yanayohusu ardhi na mipaka
Akizungumza katika kikao na wanahabari , mwenyekiti wa viongozi hao Limale Macho , amesema mkutano huo ulipangwa kwa kusudi la kutafuta suluhu baada ya tetesi kwamba kwa muda sasa ndege aina za elikopta zimekuwa zikiizunguka ardhi hiyo kwa kile kinachokisiwa na wakaazi wa LOROO kama kuchunguzwa na watu wasiojulikana wenye nia ya kutaka kujua rasilimali zilizoko ardhini humo hivo kuwatia wakaazi wasiwasi wakidai kwamba huenda kuna njama ya unyakuzi wa ardhi hiyo
Aidha Limale amehoji umuhimu wa kutafuta kisheria cheti cha ardhi hiyo almaarufu Customary Certificate ili kuzuia uwezekano wa yeyote kudai ardhi hiyo anayosema kwamba ni uridhi kutoka kwa wazee wao